Mshitakiwa kesi ya kina Mbowe aeleza alivyoteswa - NOA Swahili

Mobile Menu

Posts Title Display

Top Ads

Responsive Leaderboard Ad Area with adjustable height and width.

More News

logoblog

Mshitakiwa kesi ya kina Mbowe aeleza alivyoteswa

Dec 15, 2021
Mshtakiwa wa tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameieleza mahakama jinsi alivyokamatwa akiwa mkoani Kilimanjaro kuteswa kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Mohamed Abdillahi Ling’wenya ameiambia mahakama leo Alhamisi Novemba 25, 2021 kuwa baada ya kukamatwa alipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Moshi ambapo alifungwa pingu na kupitishiwa bomba katikati ya miguu hali iliyomfanya awe kichwa chini miguu juu. Wakili Matata anaanza kumuongoza kutoa ushahidi wa utetezi wake anasema: “Naitwa Mohamed Abdillahi Ling'wenya, naishi Kimara King'ong'o. Nilikuwa Askari wa Jeshi la Wananchi. Niliacha mwaka 2017” Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya kuacha kazi nikawa naishi Shinyanga. Baada ya Shinyanga nikapata kazi Mtwara Mshtakiwa Ling'wenya: Nilikuwa kwenye kampuni ya Mhindi. Niliacha huko nakumbuka nilipigiwa simu na Denis Urio kwamba Mbowe anahitaji ulinzi wa VIP Protection Jaji: Naomba uwe unatoa sauti ili watu wote wasikie. Mshtakiwa Ling'wenya: Tarehe 5 mwezi wa 8, 2020, nakumbuka nilikuwa Moshi. Nilivamia na askari Polisi nikawekwa kwenye gari na kupelekwa Central Police Moshi. Askari walikuwa zaidi ya wanane. Walivyotuvamia hatukujua kama ni Polisi maana hawakujitambulisha, baada ya kuingia kwenye gari na kufungwa pingu mmoja akatoa amri kwenda police Central. Mshtakiwa Ling'wenya: Nilikuwa na Adamu Hassan Kasekwa (mshtakiwa wa pili) Mshtakiwa Ling'wenya: Nawakumbuka baadhi, nakumbuka Goodluck Minja, Mahita, Jumanne, Ramadhani Kingai, ndio hao nawakumbuka kwa majina. Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya kufikishwa Moshi niliwekwa selo baada ya muda nikatolewa nikapelekwa kwenye chumba ambacho nilikuta kuna watu wengi... Ni eneo la palepale Central. Mshtakiwa Ling'wenya: Waliokuwemo humo chumbani ni wale niliowataja mwanzo na wengine sikuwafahamu. Nilikuta wana simu zao wakawa wanarekodi na nikaanza kuhojiwa nini kilichokuleta Moshi Mshtakiwa Ling'wenya: Aliyekuwa ananihoji ni Jumanne anadakia Mahita, sababu nilipokuwa najibu kuwa ni VIP protection kwa Mheshimiwa Mbowe wao wakawaa wanasema sisi tunajua kilichokuleta huku usitudanganye. Mshtakiwa Ling'wenya: Aliyeniambia hayo maneno ni Jumanne. Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya kuniambia hivyo Mahita akasema huyu si hataki kusema. Nilikuwa nimefungwa pingu, akanifunga akachukua bomba akapitisha bomba katikati ya miguu akanyanyua nikabinuka nyayo zikawa juu kichwa chini. Mshtakiwa Ling'wenya: Mahita akaanza kunipiga kwenye nyayo. Zoezi hili lilichukua makadirio kama nusu saa. Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya kupigwa pale sana na kilichokuwa kinaulizwa sasa ni kilio tu sina la kuongea. Nikasikia sauti humo nadhani ya askari kuwa msipige. Mshtakiwa Ling'wenya: Wakanifungua kisha wakaninyanyua mpaka selo. Kipindi mimi napelekwa kuadhibiwa Adamoo yeye alikuwa selo maana yeye ndo alianza kuondoka ingawa sikujua anapelekwa wapi. Alikuwa selo nyingine. Mshtakiwa Ling'wenya: Hiyo ilikuwa tarehe 5 mwezi wa 8 nilikuja kutoka tena kesho yake tarehe 6, mwezi wa 8, 2020 ambapo nilifungwa kitambaa kizito nikajua safari imeanza. Muda siwezi kukumbuka ila majira ilikuwa ni jioni sababu jua lilikuwa limeshaanza kupungua. Mshtakiwa Ling'wenya: Madai kuwa tulipofikishwa Central Police (Moshi) tulitoka tena na kuanza kuzunguka sehemu mbalimbali na polisi ni uwongo, tulivyoingia hatukutoka mpaka tulipochukuliwa na kuanza safari. Mshtakiwa Ling'wenya: Sikujua tunaenda wapi ila ilikuwa ni safari ya muda mrefu. Siwezi kusema masaa rasmi ila safari ilianza jioni na tulifika Alfajiri. Mshtakiwa Ling'wenya: Wakati tuko kwenye gari kabla sijafungwa kitambaa walikuwemo kina Goodluck na wengine walioongezeka sikuweza kuwafahamu. Mshtakiwa Ling'wenya: Hawa niliowataja niliwajua majina maana tangu walipotukamata mpaka tunapekekwa mahakamani tulikuwa nao na wakawa wanaitana majina. Mshtakiwa Ling'wenya: Njiani (kuelekea Dar) hakuna kilichotokea ila ni mimi tu nilichoka shingo nainamishwa, lakini gari kusimama popote hakuna. Mshtakiwa Ling'wenya: Mpaka hapo tayari nilikuwa nimeshajihisi ni matekwa maana nimepigwa pingu, sina uhuru wowote, nilishajihisi niko kwenye himaya yao. Mshtakiwa Ling'wenya: Tulipofika Dar bado nilikuwa nimefungwa kitambaa nikashushwa nikainamishwa hivyo na kitambaa change nikaingiza selo. Wakili Matata: Baada ya Kufika selo Mshtakiwa Ling'wenya: Waliponifikisha walinifungua kitamba cha usoni, wakanifungia. Niliposogea kwenye nondo nikaona kuna selo nyingina na kuna watu. Mshtakiwa Ling'wenya: Hao watu wakanisogelea wakanza kuniuliza nini tatizo nikawaambia nimekamatwa Moshi sijui tatizo. Mshtakiwa Ling'wenya: Yule mmoja akaniambia hapa ni Tazara na wanaoletwa hapa ni kwa tuhuma za kigaidi. Sisi unaotuona hapa ni tuhuma za ugaidi wakaniuliza ulikuwa unafanya kazi gani. Nikawaambia nilikuwa Askari Mshtakiwa Ling'wenya: Naye akasema alikuwa Askari kikosi cha Twalipo kwa Aziz Ali, alikamatwa akiwa msikitini. Mshtakiwa Ling'wenya: Pikipiki yake alikuwa ameiacha nje alipotoka msikitini akakuta imefungwa akakamatwa akapelekwa Tazara. Mshtakiwa Ling'wenya: Alipokamatwa hilo suala alikuwa halijui lakini akasema alishaambiwa ni ugaidi. Mshtakiwa Ling'wenya: Nami nilijitambulisha ni Askari wa Kikosi cha 93KJ Kikosi cha Makomando Mshtakiwa Ling'wenya: Kisha akasogea mwingine akasema yeye ni Sheikh wa Manyara. Walikwenda kumchukua wakamwachia wakamchukua tena Mshtakiwa Ling'wenya: Pale kulikuwa na askari mmoja aliyekuwa anahusika anaitwa Sajenti Kidume, nipomuomba mswaki akasema kuwa yeye hahusiki nami kwa sababu niko pale kwa maelekezo. Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya muda nilikuja kutolea selo nikapanda juu kuna chumba na nikakuta soda juu ya meza ikiwa imepambwa na kitambaa, wakaingia watu ambao nawafahamu, Alex Ahadi na Chum Chungulu nilikuwa nao kule 92 KJ. Mshtakiwa Ling'wenya: Hiyo siku ilikuwa tarehe 7, mchana Mshtakiwa Ling'wenya: Waliingia hao wawili nimapata kusalimiana nao, wakanisogelea wakaniuliza umetoke wapi nikawaambia sijui. Alex Ahadi akaniambia usiwe na wasiwasi hapa ni Polisi Tazara. Mshtakiwa Ling'wenya: Mara akaingia Mahita, Jumanne, Goodluck, Kingai akaongezeka na mtu aliyeingia na video camera. Mshtakiwa Ling'wenya: Walikuwa wananihoji jinsi nilivyompata mwenyekiti Freeman Mbowe, kilichonipeleka Moshi na nani akiyeniunganisha na Freeman Mbowe. Mshtakiwa Ling'wenya: Pale nilikuwa nikihojiwa na Omar Mahita. Mshtakiwa Ling'wenya: Niliwajibu kwamba aliyeniunganisha na Freeman Mbowe ni Denis Urio ambaye ni Luten wa Jeshi 92 KJ na kazi aliyokuwa ameniambia ni VIP Protection Mshtakiwa Ling'wenya: Kwa makadirio shughuli hiyo ya kunihoji dakika 30 hazifiki. Na aliniuliza sababu ya kwenda Moshi nikamwambia nilikuwa namfuata bosi ili tukaelewane naye. Mshtakiwa Ling'wenya: Walikuwa wananichukua video na baada ya kumaliza hilo wakanirudisha selo. Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya kurudishwa selo nilipofungiwa ndo ulikuwa mwisho wa kunifungulia. Mshtakiwa Ling'wenya: Ilipofika tarehe 8 wale wengine ambao walikuwa wanaona huko nje wakaniambia jamaa wanakuja (Askari Polisi) lakini hawakufika kwenye selo yangu. Walizunguka nyuma wakiongea na simu. Mshtakiwa Ling'wenya: Nikishawafahamu, kwanza nilimuona Good luck akaongea na simu baadaye Chuma Chungulu. Mshtakiwa Ling'wenya: Tarehe 9, nilikuwa nasikia mtu analia, nilipochungulia hivi huko nyuma nikamuona mtu nikamtambua alikuwa ni Denis Urio. Mshtakiwa Ling'wenya: Denis Urio Namfahamu nilishanya naye kazi 92, Kikosi cha Makomandoo Mshtakiwa Ling'wenya: Kule kwenye magari sikuona walichokuwa wanamfanya Urio, ila niliona anatolewa wkuwa nilishasikia sauti ya kilio kwa ufahamu wangu nilijua alikuwa anapigwa. Mshtakiwa Ling'wenya: Hiyo tarehe 9 usiku, nikafunguliwa selo, nikafugwa kitambaa, nikaingizwa kwenye gari tukaondoka. Selo alinitoa Goodluck na Mahita. Mshtakiwa Ling'wenya: Tulikokuwa tunaenda mimi sikufahamu. Mshtakiwa Ling'wenya: Safari zetu mimi na Adamoo zilikuwa za kufungwa kitambaa ila tukiwa selo tulikuwa tunaongea mfano tulipokuwa Tazara baada ya kutambua kuwa tuko selo zinazokaribiana. Mshtakiwa Ling'wenya: Tulikuwa tunasalimiana namuuliza vipi hali, mahabusu pale Tazara nilikowekwa kulikuwa kuna selo nyingine mbele yangu ndio wakaniambia mwenzako kawekwa huku, na nilipomuita kwa sauti akaitikia. Mshtakiwa Ling'wenya: Hiyo safari (ya Agosti 9, 2020) mwanzo sikuifahamu nilifungwa kitambaa lakini wakati tunaendelea huyo Goodluck akawa ananitikisa na bastola kuwa hapa usilete ujanja na nikileta usumbufu watanipoteza nitulie hivyohivyo. Mshtakiwa Ling'wenya: Tulipofika gari ikasimama wao wakashuka na baada ya muda nikasikia sauti, mshushe huyu. Mshtakiwa Ling'wenya: Nikafunguliwa mlango nikashikwa kwenye suruali nyuma nikapelekwa kaunta nikafunguliwa kitambaa ndio nikamuona kuwa ndiye huyu. Mshtakiwa Ling'wenya: Niliingizwa selo akaja Jumanne akanipa kikaratasi akaniambia kuanzia leo shika hiki kikaratasi akija mtu mwambie wew ni Johnson John, kile kikaratasi kilikuwa kimeandikwa Johnson John. Mshtakiwa Ling'wenya: Kwenye hiyo safari ndani ya gari siwezi kusema idadi kamili maana nilifungwa kitambaa, lakini niliposhuka alinishika Goodluck, akaja Jumanne na Kingai Mshtakiwa Ling'wenya: Baadaye nilikuja kufahamu pale ni Mbweni baada ya kuuliza. Kuna Askari mmoja alikuwa ni Koplo, nikamuuliza hapa ni wapi? Akasema hupajui, utapajua tu na utasema akaondoka Mshtakiwa Ling'wenya: Baadaye muda huohuo akarudi akaanza kuniuliza particulars zangu nikamwambia nilikuwa Askari 92 ( Kikosi cha Jeshi). Tulivyoongea sana akaniambia hapa ni Mbweni Polisi na kama wewe ni komando basi mmeshafika watatu. Mshtakiwa Ling'wenya: Nikamuuliza huyo wa tatu ni nani, akaniambia mmoja mmeingia naye mwingine nilipomuuliza akasema ni Luten wa Jeshi naye ni Komando. Mshtakiwa Ling'wenya: Nikamuuliza yuko yukoje huyo? Akaniambia ni mweupe anaitwa Urio jina nikamtajia Denis. Mshtakiwa Ling'wenya: Alisema huyo mwingine akijaribu kumsemesha anajificha Mshtakiwa Ling'wenya: Akaenda huko akarudi akaniambia ndiye Denis Urio, anasema yeye aliwatafutia kazi kwa nia njema tu hayo mengine hayafahamu, nikamwambia mwambie na huyo Adamu asiwe anajificha, tuwe tunasalimiana. Mshtakiwa Ling'wenya: Hivyo Tulikuwa tunasalimiana kwa sauti. Mshtakiwa Ling'wenya: Walivyoniacha pale kesho yake tarehe 10 mwezi wa 8, 2020, alikuwa anapita Mkuu wa Kituo, mwanamke. Mshtakiwa Ling'wenya: Alipofika kwangu akaniuliza unaitwa nani, nikamwambia Naitwa Johnson John. Akaniambia nini kilichokuleta huku, nikampa maelezo na kazi yangu, na kazi niliyokuwa naifuatilia mpaka nikakamatwa. Mshtakiwa Ling'wenya: Akaniambia wewe niambie jina lako la ukweli ndipo nikamwambia Mohamed Abdillahi Ling'wenya. Mshtakiwa Ling'wenya: Baada ya kumtajia majina yangu aliniahidi kuwa tutakusaidia, akaondoka mpaka asubuhi Mshtakiwa Ling'wenya: Alipoondoka yeye muda mfupi akaja Goodluck, Jumanne na Mahita waliponifungulia nikakutana na Alex Ahadi na Chuma Chungulu. Mshtakiwa Ling'wenya: Nikaingizwa kwenye chumba fulani hivi. Hicho chumba kutoka selo nilikokuwa nilitembea kwenye korido nikapishana na Urio, nikakata kona kulia na kisha kulia tena nikakutana na chumba na ndani tena kuna chumba kinaitwa Ofisi ya Upelelezi, nikaishia chumba cha nje. Mshtakiwa Ling'wenya: Nilipokataa pale, Goodluck akawa amesimama mlango akaja Jumanne na bahasha akaifungua akasema bwana hatutaki usumbufu maana kila kitu tumeshakijua. Chukua hayo makaratasi usaini. Mshtakiwa Ling'wenya: Niliangalia mlango nikamuona Goodluck amesimama na bastola akaniambia ukitaka kuleta ujanja wako tutakufanya kama tulichokuwa Moshi. Mshtakiwa Ling'wenya: Niliogopa kwa mazingira yale ya bastola na wakati nafikiria pale kusaini akapitishwa Adamu mimi nikiwa nimekaa na Jumanne. Mshtakiwa Ling'wenya: Zile karatasi alizotoa Jumanne sikupata kufahamu ni za nini hakunipa hata ruhusa ya kusoma alichotaka ni kusaini tu. Mshtakiwa Ling'wenya: Aliziweka mezani nikasaini akazirudisha tena kwenye bahasha. Mshtakiwa Ling'wenya: Nilipelekwa selo nikakaa pale. Mkuu wa kituo ananiambia tunaendelea kufuatilia Mshtakiwa Ling'wenya: Hadi Tarehe 19,2020 nikatolewa selo, nikaingizwa kwenye gari baadaye Adamu naye akaletwa, tukaingizwa na tukaambiwa tusijali haki tutaipata Mahakamani. Mshtakiwa Ling'wenya: Kuanzia Moshi hatukula chochote, safarini pia hatukupata chakula, Tazara tulifika tarehe 7 alfajili mchana tulipata ugali na mboga za majani. Mshtakiwa Ling'wenya: Jioni hatukula tena Tazara mpaka tunaondoka. Mbweni nilikuwa napata lesheni lakini si ile mahabusu wote wanapewa bali nilikuwa napewa na yule askari, mpaka tulipopelekwa Mahakamani. Mshtakiwa Ling'wenya: Mahakamani Kisutu tukiwa mahabusu, Goodluck alileta chakula wali na dagaa ndio tukala. Mshtakiwa Ling'wenya: Tangu nikiwa Moshi, Tazara na Mbweni sikuwahi kuwasiliana na mtu mwingine yeyote. Mshtakiwa Ling'wenya: Kila kituo tulichokuwa tunapelekwa nilichokuwa naomba naambiwa wewe hautuhusu na hao kina Goodluck, Jumanne ndio hawakuwa wanataka kusikia kitu chochote. Mshtakiwa Ling'wenya: Central Police Dar. Sijawahi kufika, nilikamatwa Moshi nikaletwa moja kwa moja Tazara na kila kituo nilikuwa nawekwa moja kwa moja selo sijawahi kurekodiwa kwenye kitabu chochote. Mshtakiwa Ling'wenya: Siku ile Msemwa (shahidi wa pili wa kesi ndogo) aliposema alikuwa Central na alinipokea na baadaye akahamishiwa Oysterbay na siku ileile nilimuomba wakili wangu anisaidie kuandika barua ya kwenda kwa (Kamanda wa Polis Mkoa Ilala) ili aithibitishie mahakama kwa kunipa movement order ya kwenda Oysterbay, OB ( Kitabu cha Matukio) kuangalia matukio ya siku hiyo na Station Diary kuthibitisha kuwa siku hiyo aliingia kazini. Mshtakiwa Ling'wenya: Barua hiyo aliiandika Wakili Kibatala na saini yake naifahamu kwa sababu ndiye kiongozi wa jopo la mawakili na tangu tukiwa Kisutu ndiye alikuwa anashughulika na kusaini makaratasi Mshtakiwa Ling'wenya: Nikiiona barua hiyo nitaitambua kwa kuona jina langu, namba ya kesi namba 16 ya mwaka 2021, Mhuri wa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni. Jaji: Nina wasiwasi Kuna watu wanamsaidia shahidi, Naomba wengine muwe watazamaji mumuache shahidi ajibu. Matata: Shahidi Ukijibu muangalie Jaji Kumtoa wasiwasi wa majibu yako. Wakili Matata anaendelea kumuongoza shahidi namna ya kuitambua barua hiyo na anaiomba mahakama amuoneshe shahidi barua hiyo. Mshtakiwa Ling'wenya baada ya kuangalia nakala hiyo anasema: Ndio yenyewe, nimeona Kuna kesi namba 16/2021, kingine nimeona jina langu Mohamed Abdillahi...

No comments:

Post a Comment