BEKI ya NMB imewapiga tafu wana michezo wa Visiwani Zanzibar kwa kutoa vifaa vya michezo kwa ajili ya kusherehekea miaka 56 ya Mapinduzi.
Zoezi hilo la kukabidhi vifaa hivyo limefanywa na Meneja wa NMB tawi la Zanzibar, Abdallah Duchi ambaye alimkabidhi vifaa vya michezo Salim Ali Jazira kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Vifaa hivyo ni pamoja na Jezi na Mipira kwa ajili ya michezo ya kusherehekea miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment