Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi mwingine “atapangiwa kazi nyingine” - NOA Swahili

Mobile Menu

Posts Title Display

Top Ads

Responsive Leaderboard Ad Area with adjustable height and width.

More News

logoblog

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi mwingine “atapangiwa kazi nyingine”

Mar 26, 2019


Ni habari kubwa na ya kwanza kutoka IKULU Dar es salaam leo yakiwa ni maamuzi mengine ya Kiongozi wa Nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ambapo uteuzi huu unaanza leo tarehe 26 March 2019.
Taarifa ya IKULU mapema hii imesema Rais JPM amemteua Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na anachukua nafasi ya Richard Mayongela ambae uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambako atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Ndyamukama alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam na ndiye alikuwa msimamizi Mkuu wa ujenzi wa majengo namba 3 (Terminal 3) ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam ambayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika

No comments:

Post a Comment