Kuna
mambo ambayo wataalamu wengi wamekuwa wakiongelea katika maisha hasa
yanayohusiana na hisia, tunapokuja kwenye swala la kutaka kufanya
maamuzi tunashauriwa sana kuepuka kufanya maamuzi unapokuwa na hisia
fulani, hii inaweza kukuletea matokeo chanya au hasi lakini mara nyingi
unakuwa haujategemea kupata matokeo hayo kulingana na hali uliyokuwa
nayo.
Kwa wanawake, hii huwa ngumu kwao kwa sababu kuna hali
ambazo aidha kwa kupenda au kutokupenda anaweza kujikuta tu akifanya
maamuzi bila kujali yataleta matokeo gani baadae.
Kwa
kumsikiliza pia moja ya wataalamu wa mahusiano kutoka chuo kikuu cha
Dar Es Salam , Chris Mauki anasema kuwa kuna hali ambazo mwanamke hata
ufanye nini inakuwa ngumu kwake kuacha kufanya maamuzi pengine apate mtu
wa karibu sana kuweza kuzipinga hatua zake.
Baadhi ya hali hizo zinazoweza kumfanya ashindwe kuacha kufanya maamuzi ni pamoja na :-
- Akiwa
mpweke – akiwa na kiu ya kuliwazwa kwenye upweke wake haangalii huyu ni
mume wa mtu, mchumba wa mtu, mzazi wa mtu. Yeye anachotaka upweke wake
uishe - Akiwa desparate (mwenye kiu ya kuolewa) – mwanamke akiwa
kwenye hali hii, basi mwanaume yoyote kwake ni potential husband, awe
mume wa mtu au la, akifikia hapa hajali mambo ya kupima afya, mambo ya
dini au imani, vigezo na masharti vyote vinafukiwa ardhini. - Akiwa
na kiu ya mtoto – Hapa hajaliwi mtu inajaliwa mbegu tu. Kila akiona
mwanaume anamwona kama baba mtoto wake, hapa haliangaliwi penzi tena
bali mbegu za mtoto. Hapa hata kama ana imani ya kuhamisha milima
atakuwa tayari kwenda kwa mganga pale anapoona maombi hayafanyi kazi.
Mtoto atatafutwa come what may, come sun come rain
Hali yako
na mapito yako yasikufanye ushushe standards zako. Ndio maana taji hata
siku moja haitolewi mwanzoni bali mwishoni. Yeye avumiliaye atavikwa
taji –
No comments:
Post a Comment