Wanawake Zijueni Dalili Za Wanaume Ambao Sio Waoaji - NOA Swahili

Mobile Menu

Posts Title Display

Top Ads

Responsive Leaderboard Ad Area with adjustable height and width.

More News

logoblog

Wanawake Zijueni Dalili Za Wanaume Ambao Sio Waoaji

Apr 28, 2019







                                                                           Loading...






Wahenga
wanasema raha ya mapenzi umpate akupendae ingawa watu wengi wamekuwa
wakiumizwa na mapenzi na watu wanaojulikana kama Matapeli wa mapenzi.

Wapo
ambao wamekata tamaa kabisa, hawataki kusikia kitu kinachoitwa ndoa
maana kila walipojaribu kutupa karata wamejikuta wakiambulia maumivu.
Hivyo wanaona bora kuishi kivyaovyao tu.





Ni vyema kujua dalili za mwanaume ambaye sio muoaji ambaye yupo kwa ajili ya kukuzuga:

1.Atakutafuta Wakati Wa Kukutana kimwili tu 

Yupo
kwako kwa ajili ya maslahi fulani na baada ya muda atakuacha  mtu
ambaye yupo kwako halafu hana muda na wewe zaidi ya kukuhitaji tu kwa
ajili ya kujiburudisha, huyo anza kumtilia shaka.

2. Mwanaume ambaye sio muoaji atajifanya ni mpenzi wako lakini pia hapendi umjue sana.

Hahitaji
uingie kwenye maisha yake kiundani, mnakutana tu barabarani au hotelini
biashara imeishia hapo. Hataki kukutambulisha kwa ndugu au hata
marafiki. Ukimuona yupo hivyo, anza kuwa naye makini.

3. Hatakuwa na Maongezi ya Maendeleo na wewe.

Wanaume
matapeli mara nyingi huwa wanakuwa hawapendi sana kuzungumza mipango
endelevu na watu wao. Mwanamke anapoanzisha tu habari hizo, anaruka
fasta na kuchomekea mada nyingine. Hayupo tayari, hawezi kukuvumilia
uanze kuzungumza habari za sijui kuwa na familia, kuwa na watoto na
mambo mengine kama hayo. Anataka mzungumzie zaidi viwanja vya starehe,
kula raha na kumaliza mahitaji yake ya kimwili. Baada ya hapo, hana
mpango tena na wewe.

4. Atakudanganya kila nafasi atakayopata

Ukimuona
mwanaume anakuwa muongomuongo, hana kauli moja katika maisha yenu hiyo
pia ni dalili mbaya. Mwanaume ambaye ana nia thabiti ya kuwa na wewe,
hawezi kuwa mjanjamjanja. Kama ni sanaa hizo atazifanya kwa watu wengine
lakini si kwako.




No comments:

Post a Comment