Mahakama ya katiba ya Indonesia imeiamuru serikali kuifanyia mabadiliko ndani ya miaka miwili sehemu ya sheria ya ajira iliyo na utata, ikiielezea kama sheria inayokiuka katiba.
Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka uliopita, ilisababisha maandamano makubwa nchini Indonesia kufuatia madai kuwa inakandamiza haki za wafanyakazi na kudhoofisha ulinzi wa mazingira.
Jaji Anwar Usman amesema iwapo mabadiliko hayatafanyika ndani ya miaka miwili, sheria hiyo itaorodheshwa kikamilifu kwenda kinyume cha katiba.
Serikali ya Indonesia haijasema lolote kuhusiana na uamuzi wa mahakama, lakini awali ilisema sheria hiyo inanuiwa kuongeza uwekezaji na kuimarisha ushindani katika soko la ajira
No comments:
Post a Comment