Mzee wa miaka 80 ajinyonga Dodoma - NOA Swahili

Mobile Menu

Posts Title Display

Top Ads

Responsive Leaderboard Ad Area with adjustable height and width.

More News

logoblog

Mzee wa miaka 80 ajinyonga Dodoma

Jan 27, 2022
Mkazi wa Njedengwa mkoani Dodoma, Edward Lusito anayekadiriwa kuwa na zaidi ya umri kati ya miaka 80 hadi 90 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani chumbani kwake usiku wa kuamkia leo.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Njedengwa, Daimu Haji amesema leo Alhamis Januari 27, 2022 kuwa mzee huyo alikutwa amejinyonga leo asubuhi ambapo alitumia dumu la maji kusimamia na kisha kujinyonga.


“Wanasema kuwa hawakuwa na ugomvi wowote kabla ya kujiua, wala hakuwa na shida yoyote,”amesema.


Ndugu wa marehemu Agnes Lusito amesema marehemu alikuwa akiishi na watoto wake jirani ambapo walikuwa na kawaida ya kwenda kumjulia hali kila siku wanapoamka.


Agnes amesema walipokwenda leo asubuhi kumjulia hali walikuta amejinyonga.


“Hivi karibuni alipata tatizo la macho akawa haoni. Watoto wake wanaoishi karibu ndio walikuwa wanamuangalia kihuduma,”amesema.

No comments:

Post a Comment