Rais Samia awataja wanaotuliza ubongo wake - NOA Swahili

Mobile Menu

Posts Title Display

Top Ads

Responsive Leaderboard Ad Area with adjustable height and width.

More News

logoblog

Rais Samia awataja wanaotuliza ubongo wake

Jan 27, 2022

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa wajukuu zake ndiyo tiba yake kuu pale kichwa chake kinapokuwa kimejaa kwa mambo mengi hasa akiwa Dar es Salaam.


Hayo ameyabainisha hii leo Januari 27, 2022, wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa jijini Dodoma, ambapo ametimiza umri wa miaka 62.


"Ukiona kichwa kimejaa zaidi tiba yangu ni wajukuu, napiga tu simu nileteeni hao kwahiyo wanakuja kwa masaa kadhaa hasa nikiwa Dar es Salaam, piga kelele panda shuka, pigishwa mbio kwenye ngazi wakirudi wanakokaa basi ubongo umepumzika," amesema Rais Samia

No comments:

Post a Comment